Mastering an Art of drafting Written statement of defence in swahili

JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
KATIKA BARAZA LA ARDHI NYUMBA NA MAKAZI WILAYA YA MASASI
MAOMBI NAMBA ………. YA MWAKA 2023
XXXXXXXXXXX……………………… MLETA MAOMBI
DHIDI YA
YYYYYYYYYYYYU………………… MJIBU MAOMBI
HATI YA UTETEZI

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Nyumba na Makazi naomba kuleta majibu ya mleta madai;
Kwamba, jina kamili na anunwani ya mleta maombi hakuna mgogoro.

 1. Kwamba jina kamili la Mjibu maombi ni XXXXXXXXXXXX na si zzzzz kama ilivyo kwenye hati ya madai. Anuwani ni sahihi.

2.Kwamba eneo lenye mgogoro ni jumla Ekari 3 vilivyopo Kitongoji cha Kigoma, Kijiji cha Bulima,Kata ya Nyashimo, Wilaya ya Busega.

3.Kwamba makadirio ya thamani ya eneo la mgogoro ni fedha za kitanzania kiasi cha shilingi milioni 9 [9,000,000] Tshs tofauti na madai ya Mleta maombi.

4. Kwamba, ni sahihi hakuna mgogoro wa kodi ya pango.

5.Maelezo kuhusu kiini cha mgogoro;

i. Kwamba, ni sahihi eneo bishaniwa lilikuwa lina milikiwa na marehemu Ludanha Kunyima na mke wake Salome Mhekela.
ii.Kwamba, baada ya LUDANHA KUNYIMA kufariki Shamba lilibaki mikononi mwa mke wake SALOME MHEKELA mpaka umauti ambapo aliacha wosia uliomrithisha mjibu maombi NG’WAMBA MATINDI.
iii. Kwamba, kati ya Ludanha Kunyima na Salome Mhekela hakuna aliyejaliwa kupata mtoto na hivyo kutia shaka madai ya mleta maombi.
iv.Kwamba, mjibu maombi amekuwa mmiliki halali wa eneo husika toka umauti wa Salome Mhekela. Vilevile ni miaka thelathini imepita tangu alipofariki Salome Mhekela hivyo kutia shaka madai yake ya sasa kuwa ndiye mtoto wa Ludanha Kunyima.
v. Kwamba, eneo bishaniwa ni mali halali ya NG’WAMBA MATINDI ambalo alipewa na Salome Mhekela kupitia WOSIA.

HIVYO BASI, Mjibu Maombi anaiomba Baraza hili tukufu itoe hukumu na amri dhidi ya Mleta Maombi katika nafuu zifuatazo:-
Itamkwe kwamba YYYYYYYY ni mmiliki halali wa eneo bishaniwa kutokana na vielelezo vinavyothibitisha urithishwa kutoka kwa ZZZZZZ
Gharama za shauri hili ziwe juu ya Mleta Maombi.
Nafuu yoyote ambayo Baraza hili litaona ni sawa na haki kutolewa.
Mimi, YYYYYYYYYYY nikiwa mjibu maombi katika shauri hili nathibitisha maelezo yangu ni sahihi kutokana na uwezo wa fahamu zangu.
Imethibutishwa hapa MWANZA leo tarehe ………… mwezi…………. 2022

………………………………….
MJIBU MAOMBI
Imepokelewa kwenye Baraza leo………………… mwezi………………2022

                                            ………………………………….
                                            KARANI WA BARAZA

NAKALA KWA;
mjibu maombiii

IMETAYARISHWA NA;
sheriazetu and co advocates.

box 2525,

Dar es Salaam.