How to Draft Chamber summons in swahili (Wito wa Faragha) in Tanzania

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI
KANDA YA DAR ES SALAAM
MGOGORO WA KIKAZI NA: CMA/DSM/KIN/R-989/8/
87

XXXXXXX……………..………………..…MLETA MAOMBI
DHIDI YA
YYYYY…………………………………….MJIBU MAOMBI

WITO WA FARAGHA
(Kifungu cha 87 [5] cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini [Sura ya 7, 2004], Kanuni ya 28 (1) (b) ya Taasisi za Kazi (Mwongozo wa Usuluhishi na Uamuzi) Tangazo la Serikali Na. 67, 2007, Kanuni ya 29(1) (c) ya Kanuni za Taasisi za kazi (Usuluhishi na Uamuzi) Tangazo la Serikali Na. 64, 2007 na Sheria nyingine yoyote inayohusika)

WAHUSIKA WOTE wanapaswa kufika kwenye faragha mbele ya Mhe. Msumari, Mwamuzi mnamo tarehe………………..ya mwezi………..mwaka 2013 saa…………asubuhi au muda wowote utakaopangwa na Tume ili Mleta Maombi aweze kusikilizwa kuhusu amri zifuatazo:-

Kwamba Tume hii tukufu iridhie kutengua amri yake ya tarehe 15/11/2023 ya kusikiliza shauri la msingi upande mmoja.

Kwamba, Tume hii isimamishe usikilizwaji wa shauri la msingi upande mmoja.

Kwamba, Tume hii tukufu iridhie kusikiliza pande zote mbili katika shauri la msingi ili kufikia uamuzi wa haki kwa pande zote mbili.

Nafuu nyingine yoyote ambayo Tume hii tukufu itaona ni ya haki na inafaa kutolewa.

Maombi haya yanaambatanishwa na Hati ya Kiapo cha Wakili GRATIUS MAABU kitakachosomeka pamoja na sababu nyingine ambazo zitatolewa siku ya kusikilizwa maombi haya.

Imetolewa na Kutiwa saini na Muhuri wa Tume hii, leo tarehe……………mwezi Desemba, mwaka 2023.

……………………………….
MWAMUZI

Imewasilishwa mbele ya Tume hii leo tarehe ………….mwezi Desemba, mwaka 2023.

………………………..………………..
KARANI WA TUME

Imeandaliwa na:
Sheriazetu advocates and co
P.O. Box 25,
DAR ES SALAAM.

Nakala:
Yyyyyy
DAR ES SALAAM.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI
KANDA YA DAR ES SALAAM
MGOGORO WA KIKAZI NA: CMA/DSM/KIN/R-989/8/
87

XXXXX……………..………………..…MLETA MAOMBI
DHIDI YA
YYYYYY…………………………………….MJIBU MAOMBI
HATI YA KIAPO

Mimi, GRATIUS MAABU, Wakili, Mkristu, Mwanaume na Mkazi wa Dar es Salaam NINAAPA na KUSEMA kama ifuatavyo:-
Kwamba mimi ni Wakili wa kampuni ya sheria inayomwakilisha Mleta Maombi na nafahamu fika mwenendo wa shauri hili.

Kwamba, maombi haya yanatokana na amri ya tume hii [Mhe. Msuri, Mwamuzi] iliyotolewa mnamo tarehe 15 mwezi Desemba, 2013 ya kwamba shauri hili lisikilizwe upande mmoja

Kwamba, kwa kuwa Mleta Maombi hakuridhika na amri hiyo ya kusikiliza upande mmoja pasipo uwakilishi wake hivyo basi ameona na kuamua kuwa alete maombi katika Tume hii tukufu ili aone haki yake ya kusikilizwa pia inatendeka.

Kwamba, mnamo tarehe 7/11/2013 ambapo shauri lilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa ghafla asubuhi nilipaswa kusafiri kwenda Afrika ya Kusini kumsindikiza baba yangu na wakili mkuu wa kampuni yetu ya the SoLaw Chambers (Advocates), D Senga Munga kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuvamiwa na kujeruhiwa vibaya na watu wenye nia mbaya. Nakala za barua ya kuomba kuahirisha kesi na passport zimeambatanishwa na ruhusa ya Tume inaombwa ili zisomeke kama sehemu ya hati ya kiapo.

Kwamba nilirejea tarehe 15/11/2013, baada ya Baba kufariki, majira ya usiku kwa ajili ya maandalizi ya shughuli za kuaga mwili rasmi Dar es salaam na mazishi kufanyika mkoani Kilimanjaro.

Kwamba kwa kipindi chote cha msiba ofisi ilifungwa mpaka mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja. Hivyo amri sambamba na kusikiliza shauri vilifanyika wakati mimi pamoja na wafanyakazi wenzangu wote kwa ujumla tukiwa katika kipindi cha maombolezo.

Kwamba, ili kutenda haki kwa pande zote, ni vyema na haki Tume hii tukufu ikaridhia maombi yaliyopo kwenye Wito wa Faragha.

UHAKIKI
Mimi, WAKILI GRATIUS MAABU, ninathibitisha kuwa maelezo niliyoyasema katika aya ya 1, 2, 3, 4, 5, 6 na 7 ni ya kweli kwa kadiri ya uelewa wangu.

Imethibitishwa na kutiwa sahihi leo tarehe……..mwezi Desemba mwaka 2023.
..………………….….
MUAPAJI

Kiapo hiki kimetolewa hapa Dar es Salaam
na GRATIUS MAABU Wakili ……..………………
ambaye ninamfahamu binafsi leo hii MUAPAJI
tarehe…….mwezi Desemba, 2023.

MBELE YANGU:
JINA ……………………………………
SAHIHI ……………………………………
ANUANI ……………………………………
CHEO ……………………………………

Imewasilishwa mbele ya Tume leo tarehe…………mwezi Desemba, mwaka 2023.

……………………………….
    KARANI WA TUME